Surat Hud, aya 112

11:112

فَٱسۡتَقِمۡ كَمَآ أُمِرۡتَ وَمَن تَابَ مَعَكَ وَلَا تَطۡغَوۡاْۚ إِنَّهُۥ بِمَا تَعۡمَلُونَ بَصِيرٞ ١١٢

Fastaqim kamā umirta waman tāba ma'aka walā tatghaw innahū bimā ta'malūna basīr

Basi, simama sawa sawa kama ulivyo amrishwa, wewe na wale wanao elekea kwa Mwenyezi Mungu pamoja nawe; wala msikiuke mipaka. Hakika Yeye anayaona yote myatendayo. 112

Maelezo ya chini

112 Ikiwa hii ndiyo hali ya kaumu zilio jiwa na Kitabu kutoka kwa Mwenyezi Mungu, nao wakakhitalifiana kwacho na wakakitupa, basi jilazimishe kusimama sawa sawa wewe na Waumini walio pamoja nawe kuifuata Njia Iliyo Nyooka kama alivyo kuamrisha Mwenyezi Mungu. Wala msipindukie mipaka ya uadilifu kwa kupunguza, na kupuuza, na kuzidisha, kwa kuzikalifisha nafsi zenu kwa msilo liweza. Hakika Yeye Subhanahu ameyazunguka kwa ujuzi wake yote mnayo yatenda, na atakulipeni kwayo.