Surat Hud, aya 113

11:113

وَلَا تَرۡكَنُوٓاْ إِلَى ٱلَّذِينَ ظَلَمُواْ فَتَمَسَّكُمُ ٱلنَّارُ وَمَا لَكُم مِّن دُونِ ٱللَّهِ مِنۡ أَوۡلِيَآءَ ثُمَّ لَا تُنصَرُونَ ١١٣

Walā tarkanū ilal-ladhīna zalamū fatamassakumun-nāru wamā lakum min dūnillāhi min awliyā'a thumma lā tunsarūn

Wala msiwategemee wanao dhulumu, usije ukakuguseni Moto. Wala nyinyi hamna walinzi badala ya Mwenyezi Mungu, wala tena hamtasaidiwa. 113

Maelezo ya chini

113 Wala msiwapende hata kidogo maadui wa Mwenyezi Mungu na maadui zenu walio zidhulumu nafsi zao na wakapindukia mipaka ya Mwenyezi Mungu. Wala msiwategemee, au mkapendezewa na mwendo wao, na kwa kumili huko mkastahiki adhabu ya Moto, na msimpate yeyote wa kuwatetea. Mwisho wenu mtakuwa hamtanusuriwa kwa maadui zenu kwa kuwa Mwenyezi Mungu atakutupeni na kwa kuwa nyinyi mnamtegemea adui yake!