Surat Hud, aya 111

11:111

وَإِنَّ كُلّٗا لَّمَّا لَيُوَفِّيَنَّهُمۡ رَبُّكَ أَعۡمَٰلَهُمۡۚ إِنَّهُۥ بِمَا يَعۡمَلُونَ خَبِيرٞ ١١١

Wa inna kullal lammā layuwaffiyannahum rabbuka a'mālahum innahū bimā ya'malūna khabīr

Na hakika Mola wako Mlezi atawatimilizia malipo ya vitendo vyao. Hakika Yeye anayo khabari ya wayatendayo. 111

Maelezo ya chini

111 Hapana shaka yoyote kila kikundi katika hawa Mola wako Mlezi atawalipa jaza ya vitendo vyao. Hakika Yeye Subhanahu ni Mjuzi wa ukamilifu wa kubwa na dogo wanayo yatenda, ikiwa kheri na ikiwa shari. Na atamlipa kila mmoja wapo kwa mujibu alivyo tenda.