Surat Hud, aya 10

11:10

وَلَئِنۡ أَذَقۡنَٰهُ نَعۡمَآءَ بَعۡدَ ضَرَّآءَ مَسَّتۡهُ لَيَقُولَنَّ ذَهَبَ ٱلسَّيِّـَٔاتُ عَنِّيٓۚ إِنَّهُۥ لَفَرِحٞ فَخُورٌ ١٠

Wala'in adhaqnāhu na'mā'a ba'da darrā'a massathu layaqūlanna dhahabas-sayyi'ātu 'annī innahū lafarihun fakhūr

Na tukimwonjesha neema baada ya madhara yaliyo mpata husema: Taabu zimekwisha niondokea. Hakika yeye hujitapa na kutafakhari. 10

Maelezo ya chini

10 Na tukimpa neema baada ya shida aliyo kuwa nayo yeye husema: Shida zangu zote zimekwisha niondokea, wala hazitarudi tena! Na hayo humpelekea upeo wa kufurahikia starehe za dunia, na kujifakhirisha bila ya kiasi. Moyo wake huwa umeshughulika, usimshukuru Mola wake Mlezi! Hii ndiyo hali ya binaadamu wengi, wanababaika baina ya kukata tamaa na kujitapa!