Surat Hud, aya 9

11:9

وَلَئِنۡ أَذَقۡنَا ٱلۡإِنسَٰنَ مِنَّا رَحۡمَةٗ ثُمَّ نَزَعۡنَٰهَا مِنۡهُ إِنَّهُۥ لَيَـُٔوسٞ كَفُورٞ ٩

Wala'in adhaqnal-insāna minnā rahmatan thumma naza'nāhā minhu innahū laya'ūsun kafūr

Na tukimwonjesha mtu rehema inayo toka kwetu, kisha tukamwondolea, hukata tamaa akakufuru. 9

Maelezo ya chini

9 Na katika tabia za binaadamu ni kujizamisha mwenyewe katika hali aliyo nayo. Basi tukimpa baadhi ya neema na rehema, kama vile afya nzuri, na ukunjufu wa riziki, kisha baadae tukamwondolea neema hizo, kwa mujibu wa mipango yetu, yeye hupita mipaka katika kukata tamaa kuwa neema hiyo haitorudi tena; na akapita mipaka katika kuzikufuru neema nyengine ambazo bado angali anastarehe nazo.