وَأَمَّا ثَمُودُ فَهَدَيۡنَٰهُمۡ فَٱسۡتَحَبُّواْ ٱلۡعَمَىٰ عَلَى ٱلۡهُدَىٰ فَأَخَذَتۡهُمۡ صَٰعِقَةُ ٱلۡعَذَابِ ٱلۡهُونِ بِمَا كَانُواْ يَكۡسِبُونَ ١٧
Wa ammā thamūdu fahadaynāhum fastahabbul-'amā 'alal-hudā fa akhadhathum sā'iqatul-'adhābil-hūni bimā kānū yaksibūn
Na ama Thamudi tuliwaongoza, lakini walipenda upofu kuliko uwongofu. Basi uliwachukua moto wa adhabu ya kuwafedhehi kwa sababu ya yale waliyo kuwa wakiyachuma. 17
Maelezo ya chini
17 Na ama kina Thamudi tuliwabainishia njia ya kheri na njia ya shari. Lakini wao walikhiari upotovu kuliko uwongofu, ikawatwaa radi iliyo waunguza kwa madhila na unyonge, kwa sababu ya madhambi waliyo yachuma.