Surat Fatir, aya 37

35:37

وَهُمۡ يَصۡطَرِخُونَ فِيهَا رَبَّنَآ أَخۡرِجۡنَا نَعۡمَلۡ صَٰلِحًا غَيۡرَ ٱلَّذِي كُنَّا نَعۡمَلُۚ أَوَلَمۡ نُعَمِّرۡكُم مَّا يَتَذَكَّرُ فِيهِ مَن تَذَكَّرَ وَجَآءَكُمُ ٱلنَّذِيرُۖ فَذُوقُواْ فَمَا لِلظَّٰلِمِينَ مِن نَّصِيرٍ ٣٧

Wahum yastarikhūna fīhā rabbanā akhrijnā na'mal sālihan ghayral-ladhī kunnā na'malu awalam nu'ammirkum mā yatadhakkaru fīhi man tadhakkara wajā'akumun-nadhīru fadhūqū famā liz-zālimīna min nasīr

Na humo watapiga makelele: Mola wetu Mlezi! Tutoe tufanye mema sio yale tuliyo kuwa tukiyafanya. Kwani hatukukupeni umri wa kutosha kukumbuka mwenye kukumbuka? Na akakujieni Mwonyaji? Basi onjeni! Kwani walio dhulumu hawana wa kuwanusuru. 37

Maelezo ya chini

37 Na humo watapiga makelele kuomba msaada wakisema: Mola wetu Mlezi! Tutoe humu Motoni, tupate kutenda mema siyo yale tuliyo kuwa tukiyatenda duniani. Atawaambia: Hatukukupeni fursa ya kufanya a'mali, tukaufanya mrefu umri wenu kwa muda unao mkinika mtu ndani yake kuzingatia kwa mwenye kuzingatia? Na akukujieni Mtume akakuhadharisheni na adhabu hii. Basi onjeni katika Jahannamu malipo ya udhalimu wenu. Kwani mwenye kudhulumu hapati wa kumnusuru wala kumsaidia.