إِنَّ ٱللَّهَ عَٰلِمُ غَيۡبِ ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَٱلۡأَرۡضِۚ إِنَّهُۥ عَلِيمُۢ بِذَاتِ ٱلصُّدُورِ ٣٨
Innallāha 'ālimu ghaybis-samāwāti wal-ardi innahū 'alīmu bidhātis-sudūr
Kwa hakika Mwenyezi Mungu ni Mjuzi wa siri za mbinguni na ardhi. Hakika Yeye ni Mjuzi wa yaliomo vifuani. 38
Maelezo ya chini
38 Hakika Mwenyezi Mungu anajua vyema kila kilicho fichikana katika mbingu na ardhi. Hapana chenye kufichikana kwake. Na lau ange kukubalieni akakurudisheni duniani mngeli rejea yale yale aliyo kukatazeni. Hakika Yeye Mtukufu anavijua vyema vishawishi na vivutio viliomo ndani ya vifua.