وَٱلَّذِينَ كَفَرُواْ لَهُمۡ نَارُ جَهَنَّمَ لَا يُقۡضَىٰ عَلَيۡهِمۡ فَيَمُوتُواْ وَلَا يُخَفَّفُ عَنۡهُم مِّنۡ عَذَابِهَاۚ كَذَٰلِكَ نَجۡزِي كُلَّ كَفُورٖ ٣٦
Walladhīna kafarū lahum nāru jahannama lā yuqdā 'alayhim fayamūtū walā yukhaffafu 'anhum min 'adhābihā kadhālika najzī kulla kafūr
Na walio kufuru watakuwa na Moto wa Jahannamu, hawahukumiwi wakafa, wala hawatapunguziwa adhabu yake. Hivyo ndivyo tunavyo mlipa kila mwenye kuzidi ukafiri. 36
Maelezo ya chini
36 Na walio kufuru malipo yao waliyo ahidiwa ni Moto wa Jahannamu watakao uingia. Mwenyezi Mungu hatawahukumia mauti wakafa, wala hawatapunguziwa chembe ya adhabu wakapumzika. Ni kama hivyo tunavyo mlipa kila mwenye kuendelea katika ukafiri na akaushikilia.