ثُمَّ أَوۡرَثۡنَا ٱلۡكِتَٰبَ ٱلَّذِينَ ٱصۡطَفَيۡنَا مِنۡ عِبَادِنَاۖ فَمِنۡهُمۡ ظَالِمٞ لِّنَفۡسِهِۦ وَمِنۡهُم مُّقۡتَصِدٞ وَمِنۡهُمۡ سَابِقُۢ بِٱلۡخَيۡرَٰتِ بِإِذۡنِ ٱللَّهِۚ ذَٰلِكَ هُوَ ٱلۡفَضۡلُ ٱلۡكَبِيرُ ٣٢
Thumma awrathnal-kitābal-ladhīnastafaynā min 'ibādinā faminhum zālimul linafsihī waminhum muqtasidun waminhum sābiqu bil-khayrāti bi idhnillāhi dhālika huwal-fadlul-kabīr
Kisha tumewarithisha Kitabu hao ambao tuliwateuwa miongoni mwa waja wetu. Kati yao yupo aliye jidhulumu nafsi yake, na yupo wa katikati, na yupo aliye tangulia katika mambo ya kheri, kwa idhini ya Mwenyezi Mungu. Hiyo ndiyo fadhila kuu. 32
Maelezo ya chini
32 Tena tumekifanya Kitabu hichi ni mirathi ya kurithiwa na waja wetu tulio wateuwa. Basi kati yao yupo aliye jidhulumu nafsi yake kwa kuzidi maovu yake kuliko mema yake; na yupo wa kiasi, hakupita mpaka katika maovu yake na wala hakukithirisha mema yake; na miongoni mwao yupo aliye washinda wenginewe kwa kufanya mambo ya kheri, kwa kusahilishiwa na Mwenyezi Mungu. Huko kushinda katika mambo ya kheri ndio kufuzu kukubwa mbele ya Mwenyezi Mungu.