Fa idha 'azamta fatawakkal 'alallah

Tafsiri: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani

فَبِمَا رَحۡمَةٖ مِّنَ ٱللَّهِ لِنتَ لَهُمۡۖ وَلَوۡ كُنتَ فَظًّا غَلِيظَ ٱلۡقَلۡبِ لَٱنفَضُّواْ مِنۡ حَوۡلِكَۖ فَٱعۡفُ عَنۡهُمۡ وَٱسۡتَغۡفِرۡ لَهُمۡ وَشَاوِرۡهُمۡ فِي ٱلۡأَمۡرِۖ فَإِذَا عَزَمۡتَ فَتَوَكَّلۡ عَلَى ٱللَّهِۚ إِنَّ ٱللَّهَ يُحِبُّ ٱلۡمُتَوَكِّلِينَ ١٥٩

Fabimā rahmatim minallāhi linta lahum walaw kunta fazzan ghalīzal-qalbi lanfaddū min hawlika fa'fu 'anhum wastaghfir lahum washāwirhum fil-amri fa idhā 'azamta fatawakkal 'alallāhi innallāha yuhibbul-mutawakkilīn

Basi ni kwa sababu ya rehema itokayo kwa Mwenyezi Mungu ndio umekuwa laini kwao. Na lau ungeli kuwa mkali, mwenye moyo mgumu, bila ya shaka wangeli kukimbia. Basi wasamehe, na waombee maghfira, na shauriana nao katika mambo. Na ukisha kata shauri basi mtegemee Mwenyezi Mungu. Hakika Mwenyezi Mungu huwapenda wanao mtegemea. 159

Maelezo ya chini

159 Ilikuwa ni rehema ya Mwenyezi Mungu kwako wewe (Muhammad) na kwao (Waumini) kwa kuwa wewe umekuwa laini kwao wala hukuwatolea neno la ukali kwa kukosea kwao. Na lau kuwa wewe ungeli kuwa unawachukulia kwa ukavu, na moyo mgumu wangeli kukimbia. Basi nawe yapuuze makosa yao, na waombee msamaha, na ushauriane nao katika mambo ili upate maoni yao katika mambo ambayo siyo ulio teremshiwa ufunuo, Wahyi. Ukisha funga azimio lako juu ya jambo baada ya kushauriana, basi endelea nalo na huku ukimtegemea Mwenyezi Mungu. Kwani Mwenyezi Mungu humpenda anaye mwakilisha mambo yake Yeye.

Matamshi kwa Kilatini ni msaada wa kusoma ulioandikwa na Qabas kutoka kwa Kiarabu. Jifunze herufi za Kiarabu na tajwidi kwa matamshi sahihi.

Soma Surat Al-Imran yote

Maswali

Fa idha 'azamta fatawakkal 'alallah iko wapi katika Qur'ani?

Fa idha 'azamta fatawakkal 'alallah iko katika Surat Al-Imran, 3:159.