وَمَا قَدَرُواْ ٱللَّهَ حَقَّ قَدۡرِهِۦ وَٱلۡأَرۡضُ جَمِيعٗا قَبۡضَتُهُۥ يَوۡمَ ٱلۡقِيَٰمَةِ وَٱلسَّمَٰوَٰتُ مَطۡوِيَّٰتُۢ بِيَمِينِهِۦۚ سُبۡحَٰنَهُۥ وَتَعَٰلَىٰ عَمَّا يُشۡرِكُونَ ٦٧
Wamā qadarullāha haqqa qadrihī wal-ardu jamī'an qabdatuhū yawmal-qiyāmati was-samāwātu matwiyyātu biyamīnihī subhānahū wata'ālā 'ammā yushrikūn
Na wala hawakumhishimu Mwenyezi Mungu kama anavyo stahiki kadiri yake. Na Siku ya Kiyama ardhi yote itakuwa mkononi mwake, na mbingu zitakunjwa katika mkono wake wa kuume. Subhanahu wa Taa'la Ametakasika na Ametukuka na hayo wanayo mshirikisha nayo. 67
Maelezo ya chini
67 Washirikina hawakumtukuza Mwenyezi Mungu kama anavyo stahiki utukufu wake, wala hawakumjua kama anavyo stahiki kujuulikana, kwa kuwa wamemshirikisha pamoja naye wenginewe, na wakamtaka Mtume naye aingie katika ushirikina, na hali ardhi yote ni milki yake Siku ya Kiyama, na mbingu zitakuwa zimekunjwa, kama zinavyo kunjwa nguo, katika mkono wake wa kulia. Mwenyezi Mungu ametakasika na kila upungufu, na ametukuka vikubwa mno na vyote hivyo wanavyo mshirikisha naye.