Surat Az-Zumar, aya 68

39:68

وَنُفِخَ فِي ٱلصُّورِ فَصَعِقَ مَن فِي ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَمَن فِي ٱلۡأَرۡضِ إِلَّا مَن شَآءَ ٱللَّهُۖ ثُمَّ نُفِخَ فِيهِ أُخۡرَىٰ فَإِذَا هُمۡ قِيَامٞ يَنظُرُونَ ٦٨

Wanufikha fis-sūri fasa'iqa man fis-samāwāti waman fil-ardi illā man shā'allāhu thumma nufikha fīhi ukhrā fa idhā hum qiyāmun yanzurūn

Na litapulizwa barugumu, wazimie waliomo mbinguni na waliomo katika ardhi, isipo kuwa aliye mtaka Mwenyezi Mungu. Kisha litapulizwa mara nyengine. Hapo watainuka wawe wanangojea. 68

Maelezo ya chini

68 Na litapulizwa barugumu kwa yakini, na watakufa walioko mbinguni na katika ardhi ila anaye mtaka Mwenyezi Mungu kumuakhirisha mpaka wakati mwengine. Kisha litapulizwa mara nyengine, na hapo wote watainuka kutoka makaburini mwao, wakingojea watafanywa nini? Hilo barugumu (S'ur) kilugha, ni tarumbeta, mbiu, siwa, parapanda. Barugumu inalo tusimulia Qur'ani ni katika mambo ya ulimwengu usio onekana, hatujui lilivyo na hakika yake.