وَنَادَىٰ فِرۡعَوۡنُ فِي قَوۡمِهِۦ قَالَ يَٰقَوۡمِ أَلَيۡسَ لِي مُلۡكُ مِصۡرَ وَهَٰذِهِ ٱلۡأَنۡهَٰرُ تَجۡرِي مِن تَحۡتِيٓۚ أَفَلَا تُبۡصِرُونَ ٥١
Wanādā fir'awnu fī qawmihī qāla yāqawmi alaysa lī mulku misra wahādhihil-anhāru tajrī min tahtī afalā tubsirūn
Na Firauni alitangaza kwa watu wake, akisema: Enyi watu wangu! Kwani mimi sinao huu ufalme wa Misri, na hii mito inapita chini yangu? Je! Hamwoni? 51
Maelezo ya chini
51 Firauni akawatangazia watu wake kutangaza nguvu zake na madaraka yake: Kwani huu ufalme wa Misri si wangu mimi peke yangu, wala hapana mwenginewe, na hii mito ambayo mnaiona inapita chini ya jumba langu? Hamyaoni haya? Basi hamzingatii mnayo yaona ya nguvu zangu na udhaifu wa Musa? Na Firauni alitaka kwa wito wake kuutia imara ut'iifu wao.