وَٱصۡبِرۡ لِحُكۡمِ رَبِّكَ فَإِنَّكَ بِأَعۡيُنِنَاۖ وَسَبِّحۡ بِحَمۡدِ رَبِّكَ حِينَ تَقُومُ ٤٨
Wasbir lihukmi rabbika fa innaka bi a'yuninā wasabbih bihamdi rabbika hīna taqūm
Na ingojee hukumu ya Mola wako Mlezi. Kwani wewe hakika uko mbele ya macho yetu, na mtakase kwa kumsifu Mola wako Mlezi unapo simama, 48
Maelezo ya chini
48 Wewe isubirie hukumu ya Mola wako Mlezi ya kuwapa muhula hao, na wewe kupata maudhi yao. Kwani hakika wewe umo katika hifadhi yetu na ulinzi wetu. Basi vitimbi vyao havitokudhuru wewe. Na mtakase kwa kumsifu Mola wako Mlezi unapo amka.