Surat At-Tawbah, aya 97

9:97

ٱلۡأَعۡرَابُ أَشَدُّ كُفۡرٗا وَنِفَاقٗا وَأَجۡدَرُ أَلَّا يَعۡلَمُواْ حُدُودَ مَآ أَنزَلَ ٱللَّهُ عَلَىٰ رَسُولِهِۦۗ وَٱللَّهُ عَلِيمٌ حَكِيمٞ ٩٧

Al-a'rābu ashaddu kufran wanifāqan wa ajdaru allā ya'lamū hudūda mā anzalallāhu 'alā rasūlihī wallāhu 'alīmun hakīm

Mabedui wamezidi sana katika ukafiri na unaafiki, na wameelekea zaidi kutojua mipaka ya aliyo yateremsha Mwenyezi Mungu juu ya Mtume wake. Na Mwenyezi Mungu ni Mjuzi Mwenye hikima. 97

Maelezo ya chini

97 Mabedui, Waarabu wa majangwani, ndio wakubwa wa kuikataa Haki na wa unaafiki. Hao hakika wamefika upeo wa mwisho katika hayo. Na hayo ni hivyo kwa kuwa wao wapo mbali na maarifa na mwahali mwenye vitovu vya ilimu. Na wao ndio wameelekea zaidi kuwa wasiijue mipaka ya Mwenyezi Mungu, na aliyo mteremshia Mtume wake katika sharia na hukumu. Na Mwenyezi Mungu ni Mjuzi wa pande zote mbili, na ni Mwenye hikima katika malipo anayo yakadiria.