Surat At-Tawbah, aya 98

9:98

وَمِنَ ٱلۡأَعۡرَابِ مَن يَتَّخِذُ مَا يُنفِقُ مَغۡرَمٗا وَيَتَرَبَّصُ بِكُمُ ٱلدَّوَآئِرَۚ عَلَيۡهِمۡ دَآئِرَةُ ٱلسَّوۡءِۗ وَٱللَّهُ سَمِيعٌ عَلِيمٞ ٩٨

Waminal-a'rābi man yattakhidhu mā yunfiqu maghraman wayatarabbasu bikumud-dawā'ira 'alayhim dā'iratus-saw'i wallāhu samī'un 'alīm

Na katika Mabedui hao wapo wanao fikiri kuwa wanayo yatoa ni gharama ya bure, na wanakungojeleeni mambo yakugeukieni. Mageuko maovu yatakuwa juu yao! Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusikia Mwenye kujua. 98

Maelezo ya chini

98 Na baadhi ya hawa wanaafiki katika watu wa majangwani wanaona kuwa wanacho kitoa katika Sabiili-Llahi (Njia ya Mwenyezi Mungu) kuwa ni gharama na khasara ya bure, kwa kuwa vile hawaamini kuwa kuna malipo ya Mwenyezi Mungu Mtukufu. Nao wanataraji na wanangojea hali ya vita ikugeukieni nyinyi Waumini. Bali hayo mageuko yatawageukia wao! Na hiyo shari wanayo ingojea ikufikieni itawafika wao iwazunguke! Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kuzisikia kauli zao, na Mwenye kuvijua vitendo vyao na niya zao, na madhambi wanayo yachuma.