ٱلۡمُنَٰفِقُونَ وَٱلۡمُنَٰفِقَٰتُ بَعۡضُهُم مِّنۢ بَعۡضٖۚ يَأۡمُرُونَ بِٱلۡمُنكَرِ وَيَنۡهَوۡنَ عَنِ ٱلۡمَعۡرُوفِ وَيَقۡبِضُونَ أَيۡدِيَهُمۡۚ نَسُواْ ٱللَّهَ فَنَسِيَهُمۡۚ إِنَّ ٱلۡمُنَٰفِقِينَ هُمُ ٱلۡفَٰسِقُونَ ٦٧
Al-munāfiqūna wal-munāfiqātu ba'duhum mim ba'din ya'murūna bil-munkari wayanhawna 'anil-ma'rūfi wayaqbidūna aydiyahum nasullāha fanasiyahum innal-munāfiqīna humul-fāsiqūn
Wanaume wanaafiki na wanawake wanaafiki, wote ni hali moja. Huamrisha maovu na huyakataza mema, na huifumba mikono yao. Wamemsahau Mwenyezi Mungu, basi na Yeye pia amewasahau. Hakika wanaafiki ndio wapotofu. 67
Maelezo ya chini
67 Wanaafiki wanaume na wanaafiki wanawake wamefanana kwa kuwa wote wanatenda maovu, na wanayaamrisha, na wanaiacha Haki na wanaikataza, na wanafanya ubakhili kutumia mali katika njia za kheri. Basi hao kama ni viungo vya mwili mmoja. Wamemwacha Mwenyezi Mungu, na Mwenyezi Mungu naye akawaacha wala hawaongoi, kwa kuwa wao wamekwisha toka kwenye ut'iifu wa Mwenyezi Mungu.