لَا تَعۡتَذِرُواْ قَدۡ كَفَرۡتُم بَعۡدَ إِيمَٰنِكُمۡۚ إِن نَّعۡفُ عَن طَآئِفَةٖ مِّنكُمۡ نُعَذِّبۡ طَآئِفَةَۢ بِأَنَّهُمۡ كَانُواْ مُجۡرِمِينَ ٦٦
Lā ta'tadhirū qad kafartum ba'da īmānikum in na'fu 'an tā'ifatim minkum nu'addhib tā'ifata bi annahum kānū mujrimīn
Msitoe udhuru; mmekwisha kufuru baada ya kuamini kwenu! Tukilisamehe kundi moja kati yenu, tutaliadhibu kundi jingine kwa kuwa wao ni wakosefu. 66
Maelezo ya chini
66 Msitoe udhuru kama huu wa uwongo! Ukafiri wenu umekwisha dhihiri baada ya kujidai kwenu kuwa mmeamini. Na ikiwa Sisi tutalisamehe kundi moja lenu lilio tubu na likaamini, kwa sababu ya kutubu kwake kwa kweli, na kuamini kwake, vile vile tutaliadhibu kundi jengine katika nyinyi kwa kushikilia kwake ukafiri na unaafiki, na ukhalifu wake katika haki ya Mtume na ya Waumini.