إِنَّمَا يَعۡمُرُ مَسَٰجِدَ ٱللَّهِ مَنۡ ءَامَنَ بِٱللَّهِ وَٱلۡيَوۡمِ ٱلۡأٓخِرِ وَأَقَامَ ٱلصَّلَوٰةَ وَءَاتَى ٱلزَّكَوٰةَ وَلَمۡ يَخۡشَ إِلَّا ٱللَّهَۖ فَعَسَىٰٓ أُوْلَٰٓئِكَ أَن يَكُونُواْ مِنَ ٱلۡمُهۡتَدِينَ ١٨
Innamā ya'muru masājidallāhi man āmana billāhi wal-yawmil-ākhiri wa aqāmas-salawāta wa ātaz-zakawāta walam yakhsha illallāha fa'asā ulā'ika an yakūnū minal-muhtadīn
Hakika wanao amirisha misikiti ya Mwenyezi Mungu ni wale wanao muamini Mwenyezi Mungu, na Siku ya Mwisho, na wakashika Swala, na wakatoa Zaka, na wala hawamchi ila Mwenyezi Mungu. Basi huenda hao wakawa katika waongofu. 18
Maelezo ya chini
18 Lakini wanao amirisha Misikiti ya Mwenyezi Mungu ni wale wenye kumuamini Mwenyezi Mungu Mmoja peke yake, na wakasadiki kuwapo kufufuliwa na kulipwa, na wakatimiza Swala kama itakikanavyo, na wakatoa Zaka ya mali yao, na wala hawamwogopi ila Mwenyezi Mungu peke yake. Na hao ndio wanao tarajiwa kuwa mbele ya Mwenyezi Mungu waongofu wa kufuata Njia Iliyo Nyooka.