۞ أَجَعَلۡتُمۡ سِقَايَةَ ٱلۡحَآجِّ وَعِمَارَةَ ٱلۡمَسۡجِدِ ٱلۡحَرَامِ كَمَنۡ ءَامَنَ بِٱللَّهِ وَٱلۡيَوۡمِ ٱلۡأٓخِرِ وَجَٰهَدَ فِي سَبِيلِ ٱللَّهِۚ لَا يَسۡتَوُۥنَ عِندَ ٱللَّهِۗ وَٱللَّهُ لَا يَهۡدِي ٱلۡقَوۡمَ ٱلظَّٰلِمِينَ ١٩
Aja'altum siqāyatal-hājji wa'imāratal-masjidil-harāmi kaman āmana billāhi wal-yawmil-ākhiri wajāhada fī sabīlillāhi lā yastawūna 'indallāhi wallāhu lā yahdil-qawmaz-zālimīn
Je, mnafanya kuwanywesha maji Mahujaji na kuamirisha Msikiti Mtakatifu ni sawa na mwenye kumuamini Mwenyezi Mungu, na Siku ya Mwisho, na akapigana Jihadi katika Njia ya Mwenyezi Mungu? Hawawi sawa mbele ya Mwenyezi Mungu. Na Mwenyezi Mungu hawaongoi watu madhaalimu. 19
Maelezo ya chini
19 Haifalii kuwafanya washirikina wanao wanywesha maji Mahujaji, na wakauamirisha Msikiti Mtakatifu (wa Makka), katika cheo kama cha wanao muamini Mwenyezi Mungu Mmoja, na wakasadiki kufufuliwa na kulipwa kwa wayatendayo, na wakapigana Jihadi katika Njia ya Mwenyezi Mungu..Hao si makamu mamoja mbele ya Mwenyezi Mungu. Na Mwenyezi Mungu hawaongoi kwenye Njia ya kheri watu ambao wameshikilia kujidhulumu wenyewe kwa ukafiri wao, na wakawadhulumu wengineo kwa maudhi yasio kwisha.