Surat At-Tawbah, aya 17

9:17

مَا كَانَ لِلۡمُشۡرِكِينَ أَن يَعۡمُرُواْ مَسَٰجِدَ ٱللَّهِ شَٰهِدِينَ عَلَىٰٓ أَنفُسِهِم بِٱلۡكُفۡرِۚ أُوْلَٰٓئِكَ حَبِطَتۡ أَعۡمَٰلُهُمۡ وَفِي ٱلنَّارِ هُمۡ خَٰلِدُونَ ١٧

Mā kāna lil-mushrikīna an ya'murū masājidallāhi shāhidīna 'alā anfusihim bil-kufri ulā'ika habitat a'māluhum wafin-nāri hum khālidūn

Haiwi kuwa makafiri ndio waamirishe misikiti ya Mwenyezi Mungu, hali wanajishuhudishia wenyewe ukafiri. Hao ndio ambao vitendo vyao vimeharibika, na katika Moto watadumu. 17

Maelezo ya chini

17 Hawawi washirikina ndio wenye kufaa kuamirisha Misikiti ya Mwenyezi Mungu, na hali wao wangali kuendelea na ukafiri wao, na wanautangaza khasa! Vitendo vyao washirikina havitiwi hisabuni, wala hawatolipwa thawabu kwavyo! Wao ni wenye kudumu Motoni Siku ya Kiyama.