Surat Ash-Shura, aya 48

42:48

فَإِنۡ أَعۡرَضُواْ فَمَآ أَرۡسَلۡنَٰكَ عَلَيۡهِمۡ حَفِيظًاۖ إِنۡ عَلَيۡكَ إِلَّا ٱلۡبَلَٰغُۗ وَإِنَّآ إِذَآ أَذَقۡنَا ٱلۡإِنسَٰنَ مِنَّا رَحۡمَةٗ فَرِحَ بِهَاۖ وَإِن تُصِبۡهُمۡ سَيِّئَةُۢ بِمَا قَدَّمَتۡ أَيۡدِيهِمۡ فَإِنَّ ٱلۡإِنسَٰنَ كَفُورٞ ٤٨

Fa in a'radū famā arsalnāka 'alayhim hafīzan in 'alayka illal-balāghu wa innā idhā adhaqnal-insāna minnā rahmatan fariha bihā wa in tusibhum sayyi'atu bimā qaddamat aydīhim fa innal-insāna kafūr

Na wakipuuza, basi Sisi hatukukupeleka ili uwe mwangalizi wao. Si juu yako ila kufikisha Ujumbe tu. Na hakika Sisi tukimwonjesha mtu rehema kutoka kwetu, huifurahia. Na akisibiwa na ovu kwa sababu ya iliyo yatanguliza mikono yao, basi hakika mtu huyu anakufuru. 48

Maelezo ya chini

48 Wakipuuza washirikina kukuitikia wewe, ewe Mtume, basi usihuzunike. Kwani wewe si mwangalizi wao kwa hayo wanayo yatenda. Wewe umelazimishwa kufikisha Ujumbe tu, na hayo umeyabainisha wazi. Na tabia ya watu tukiwapa wasaa hupanda kiburi. Na ukiwasibu msiba kwa sababu ya maasi yao, mara wanasahau neema, wanahuzunika kwa kuteremkiwa na balaa, na wanaingia katika kufuru.