ٱسۡتَجِيبُواْ لِرَبِّكُم مِّن قَبۡلِ أَن يَأۡتِيَ يَوۡمٞ لَّا مَرَدَّ لَهُۥ مِنَ ٱللَّهِۚ مَا لَكُم مِّن مَّلۡجَإٖ يَوۡمَئِذٖ وَمَا لَكُم مِّن نَّكِيرٖ ٤٧
Istajībū lirabbikum min qabli an ya'tiya yawmul lā maradda lahū minallāhi mā lakum mim malja'in yawma'idhin wamā lakum min nakīr
Muitikieni Mola wenu Mlezi kabla haijafika siku isiyo epukika itokayo kwa Mwenyezi Mungu. Siku hiyo hamtakuwa pa kukimbilia wala hamtakuwa na cha kukingia. 47
Maelezo ya chini
47 Enyi watu! Kimbilieni kuitikia aliyo kuitieni Mtume wa Mwenyezi Mungu aliye kuumbeni na akakuleeni, nayo ni Imani na Ut'iifu, kabla uhai haujamaliza fursa ya kutenda vitendo, na ikafika Siku ya Hisabu ambayo Mwenyezi Mungu hairudishi nyuma tena baada ya kwisha ihukumia. Siku hiyo hamtakuwa na pa kukimbilia pa kukuhamini na adhabu, wala hapana cha kuzuia kitakacho kufikieni.