Surat Ash-Shura, aya 45

42:45

وَتَرَىٰهُمۡ يُعۡرَضُونَ عَلَيۡهَا خَٰشِعِينَ مِنَ ٱلذُّلِّ يَنظُرُونَ مِن طَرۡفٍ خَفِيّٖۗ وَقَالَ ٱلَّذِينَ ءَامَنُوٓاْ إِنَّ ٱلۡخَٰسِرِينَ ٱلَّذِينَ خَسِرُوٓاْ أَنفُسَهُمۡ وَأَهۡلِيهِمۡ يَوۡمَ ٱلۡقِيَٰمَةِۗ أَلَآ إِنَّ ٱلظَّٰلِمِينَ فِي عَذَابٖ مُّقِيمٖ ٤٥

Watarāhum yu'radūna 'alayhā khāshi'īna minadh-dhulli yanzurūna min tarfin khafiyyin waqālal-ladhīna āmanū innal-khāsirīnal-ladhīna khasirū anfusahum wa ahlīhim yawmal-qiyāmati alā innaz-zālimīna fī 'adhābim muqīm

Na utawaona wanapelekwa kwenye Moto, nao wamenyenyekea kwa unyonge, wanatazama kwa mtazamo wa kificho. Na walio amini watasema: Hakika wapatao khasara ni hao walio khasiri nafsi zao na ahali zao Siku ya Kiyama. Ama hakika wenye kudhulumu watakuwa katika adhabu ya daima. 45

Maelezo ya chini

45 Na kadhaalika, utawaona walio dhulumu, wakipelekwa Motoni, wamenywea kwa sababu ya unyonge ulio tokana na hivyo vitisho walivyo vikuta, wakitupia jicho kwa kificho kwenye huo Moto kwa kuukhofu vituko vyake. Na hapo Waumini watasema: Hakika walio khasiri kweli ni hao walio dhulumu nafsi zao kwa ukafiri wao, na wakawakhasiri wake zao na watoto wao na jamaa zao kwa mfarakano walio usabibisha baina yao. Na Mwenyezi Mungu ananabihisha kwamba wenye kudhulumu watakuwa katika adhabu ya milele.