وَمَن يُضۡلِلِ ٱللَّهُ فَمَا لَهُۥ مِن وَلِيّٖ مِّنۢ بَعۡدِهِۦۗ وَتَرَى ٱلظَّٰلِمِينَ لَمَّا رَأَوُاْ ٱلۡعَذَابَ يَقُولُونَ هَلۡ إِلَىٰ مَرَدّٖ مِّن سَبِيلٖ ٤٤
Waman yudlilillāhu famā lahū min waliyyim mim ba'dihī wataraz-zālimīna lammā ra'awul-'adhāba yaqūlūna hal ilā maraddim min sabīl
Na ambaye Mwenyezi Mungu amemwacha kupotea, hana mlinzi baada yake. Na utawaona wenye kudhulumu watakapo iona adhabu wanasema: Je! Ipo njia ya kurudi? 44
Maelezo ya chini
44 Na mwenye kuipotea Njia ya Uwongofu kwa kuwa hana ujuzi mwema, basi hana wa kumnusuru isipo kuwa Mwenyezi Mungu, ndiye wa kumwongoa na wa kumkinga na adhabu. Na, ewe unaye semezwa! Utaona Siku ya Kiyama wale wenye kudhulumu watakapo iona adhabu ya Akhera wanamuuliza Mola wao Mlezi, watumie mbinu gani wapate kurejea duniani, ili wapate kutenda mema, siyo waliyo kuwa wakiyatenda kwanza?