Surat Ash-Shura, aya 43

42:43

وَلَمَن صَبَرَ وَغَفَرَ إِنَّ ذَٰلِكَ لَمِنۡ عَزۡمِ ٱلۡأُمُورِ ٤٣

Walaman sabara waghafara inna dhālika lamin 'azmil-umūr

Na anaye subiri, na akasamehe, hakika hayo ni katika mambo ya kuazimiwa. 43

Maelezo ya chini

43 Ninaapa: Bila ya shaka, mwenye kuvumilia kudhulumiwa, akamwachilia aliye mdhulumu, wala asiitetee nafsi yake, pindi ikiwa huko kusamehe kwenyewe hakuupalilii ufisadi ukapata nguvu katika nchi, hakika hayo ni katika mambo ambayo yanatakikana mwenye akili ajilazimishe kuyatenda.