وَلَقَدۡ سَبَقَتۡ كَلِمَتُنَا لِعِبَادِنَا ٱلۡمُرۡسَلِينَ ١٧١
Walaqad sabaqat kalimatunā li'ibādinal-mursalīn
Na bila ya shaka neno letu lilikwisha tangulia kwa waja wetu walio tumwa. 171
Maelezo ya chini
171 Ninaapa! Hukumu yetu kwa Mitume tulio watuma imekwisha tolewa mbele, ya kwamba ushindi na matokeo mema ni yao wao dhidi ya makafiri.