Surat Ar-Ra'd, aya 15

13:15

وَلِلَّهِۤ يَسۡجُدُۤ مَن فِي ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَٱلۡأَرۡضِ طَوۡعٗا وَكَرۡهٗا وَظِلَٰلُهُم بِٱلۡغُدُوِّ وَٱلۡأٓصَالِ۩ ١٥

Walillāhi yasjudu man fis-samāwāti wal-ardi taw'an wakarhan wazilāluhum bil-ghuduwwi wal-āsāl

Na viliomo mbinguni na katika ardhi vinamsujudia Mwenyezi Mungu tu vikitaka visitake. Na pia vivuli vyao asubuhi na jioni. 15

Maelezo ya chini

15 Na vyote viliomo mbinguni na duniani, vitu, watu, majini, na Malaika, vinamnyenyekea Mwenyezi Mungu kwa matakwa yake na utukufu wake, vikitaka visitake. Hata vivuli vyao kadhaalika, vikirefuka na kufupika kwa mujibu wa nyakati za mchana adhuhuri na jioni, kwa kufuata anavyo amrisha Mwenyezi Mungu na anavyo kataza.