لَهُۥ دَعۡوَةُ ٱلۡحَقِّۚ وَٱلَّذِينَ يَدۡعُونَ مِن دُونِهِۦ لَا يَسۡتَجِيبُونَ لَهُم بِشَيۡءٍ إِلَّا كَبَٰسِطِ كَفَّيۡهِ إِلَى ٱلۡمَآءِ لِيَبۡلُغَ فَاهُ وَمَا هُوَ بِبَٰلِغِهِۦۚ وَمَا دُعَآءُ ٱلۡكَٰفِرِينَ إِلَّا فِي ضَلَٰلٖ ١٤
Lahū da'watul-haqqi walladhīna yad'ūna min dūnihī lā yastajībūna lahum bishay'in illā kabāsiti kaffayhi ilal-mā'i liyablugha fāhu wamā huwa bibālighihī wamā du'ā'ul-kāfirīna illā fī dalāl
Wa kuombwa kweli ni Yeye tu. Na hao wanao waomba badala yake hawawajibu chochote; bali ni kama mwenye kunyoosha viganja vyake kwenye maji ili yafike kinywani mwake, lakini hayafiki. Na maombi ya makafiri hayako ila katika upotovu. 14
Maelezo ya chini
14 Na hayo masanamu wanayo yaomba kwa woga na kutafuta amani badala ya Mwenyezi Mungu pekee hayawajibu wito na maombi yao. Hali yao ni kama mwenye kukunjua kiganja chake akinge maji ya kunywa na kiganja kisifike mdomoni. Na hali yao ikiwa ni hii, basi hizo dua zao haziwi ila kupotea na kukhasirika.