Surat An-Nur, aya 59

24:59

وَإِذَا بَلَغَ ٱلۡأَطۡفَٰلُ مِنكُمُ ٱلۡحُلُمَ فَلۡيَسۡتَـٔۡذِنُواْ كَمَا ٱسۡتَـٔۡذَنَ ٱلَّذِينَ مِن قَبۡلِهِمۡۚ كَذَٰلِكَ يُبَيِّنُ ٱللَّهُ لَكُمۡ ءَايَٰتِهِۦۗ وَٱللَّهُ عَلِيمٌ حَكِيمٞ ٥٩

Wa idhā balaghal-atfālu minkumul-huluma falyasta'dhinū kamasta'dhanal-ladhīna min qablihim kadhālika yubayyinullāhu lakum āyātihī wallāhu 'alīmun hakīm

Na watoto wanapo fikilia umri wa kubaalighi basi nawatake ruhusa, kama walivyo taka ruhusa wa kabla yao. Hivyo ndivyo anavyo kubainishieni Mwenyezi Mungu Aya zake, na Mwenyezi Mungu ni Mjuzi Mwenye hikima. 59

Maelezo ya chini

59 Na vijana vyenu wakifikilia umri wa kubalighi inawapasa watake ruhusa ya kuingia kila nyumba, na kila wakati, kama ilivyo wapasa wenzao wa kabla yao. Na kwa mfano wa uwazi kama huu Mwenyezi Mungu anakuwekeeni wazi Aya zake alizo ziteremsha. Na Mwenyezi Mungu Subhanahu ni Mkunjufu wa ujuzi, Mkubwa wa hikima. Anajua linalo wasilihi waja wake, na anawaatungia Sharia zinazo wanasibu, na kwa kadri ya haja yao.