وَٱلۡقَوَٰعِدُ مِنَ ٱلنِّسَآءِ ٱلَّٰتِي لَا يَرۡجُونَ نِكَاحٗا فَلَيۡسَ عَلَيۡهِنَّ جُنَاحٌ أَن يَضَعۡنَ ثِيَابَهُنَّ غَيۡرَ مُتَبَرِّجَٰتِۭ بِزِينَةٖۖ وَأَن يَسۡتَعۡفِفۡنَ خَيۡرٞ لَّهُنَّۗ وَٱللَّهُ سَمِيعٌ عَلِيمٞ ٦٠
Wal-qawā'idu minan-nisā'il-lātī lā yarjūna nikāhan falaysa 'alayhinna junāhun an yada'na thiyābahunna ghayra mutabarrijāti bizīnatin wa an yasta'fifna khayrul lahunna wallāhu samī'un 'alīm
Na wanawake wazee wasio taraji kuolewa, si vibaya kwao kupunguza nguo zao, bila ya kujishaua kwa mapambo. Na wakijihishimu ni bora kwao. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusikia, Mwenye kujua. 60
Maelezo ya chini
60 Na wanawake wakongwe ambao hawatumai kuolewa, hawalaumiwi wakipunguza baadhi ya nguo zao, kwa sharti wasiwe wanajishauwa kwa kuonyesha uzuri wa mwili wao ambao Mwenyezi Mungu ameamrisha usitiriwe. Lakini kujihishimu kwa kujisitiri kwa ukamilifu ni bora kwao kuliko kujifunua. Na Mwenyezi Mungu anawasikia wayasemayo, na anayajua makusudio yao, na atawalipa kwa hayo.