إِنَّ ٱلَّذِينَ يُحِبُّونَ أَن تَشِيعَ ٱلۡفَٰحِشَةُ فِي ٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ لَهُمۡ عَذَابٌ أَلِيمٞ فِي ٱلدُّنۡيَا وَٱلۡأٓخِرَةِۚ وَٱللَّهُ يَعۡلَمُ وَأَنتُمۡ لَا تَعۡلَمُونَ ١٩
Innal-ladhīna yuhibbūna an tashī'al-fāhishatu fil-ladhīna āmanū lahum 'adhābun alīmun fid-dunyā wal-ākhirati wallāhu ya'lamu wa antum lā ta'lamūn
Kwa hakika wale wanao penda uenee uchafu kwa walio amini, watapata adhabu chungu katika dunia na Akhera. Na Mwenyezi Mungu anajua na nyinyi hamjui. 19
Maelezo ya chini
19 Hakika hao wanao penda kutangaza machafu, wakayatangaza baina ya Waumini watapata adhabu yenye kutia uchungu duniani kwa mateso yaliyo kwisha pasishwa, na Akhera watatiwa Motoni ikiwa hawato tubu. Na Mwenyezi Mungu anazijua vyema hali zenu zote, za dhaahiri na zilizo fichikana. Na nyinyi hamjui anayo yajua Yeye.