وَلَوۡلَا فَضۡلُ ٱللَّهِ عَلَيۡكُمۡ وَرَحۡمَتُهُۥ وَأَنَّ ٱللَّهَ رَءُوفٞ رَّحِيمٞ ٢٠
Walawlā fadlullāhi 'alaykum warahmatuhū wa annallāha ra'ūfur rahīm
Na lau kuwa si fadhila ya Mwenyezi Mungu juu yenu na rehema yake, na kuwa hakika Mwenyezi Mungu ni Mpole, Mwenye kurehemu. 20
Maelezo ya chini
20 Na lau kuwa si fadhila ya Mwenyezi Mungu juu yenu na rehema yake kwenu, na kuwa Yeye ni Mwingi wa upole, Mkunjufu wa rehema, asingeli kubainishieni hukumu, na angeli kuleteeni mateso kwa haraka hapa duniani kwa maasi yenu.