Surat An-Nur, aya 18

24:18

وَيُبَيِّنُ ٱللَّهُ لَكُمُ ٱلۡأٓيَٰتِۚ وَٱللَّهُ عَلِيمٌ حَكِيمٌ ١٨

Wayubayyinullāhu lakumul-āyāti wallāhu 'alīmun hakīm

Na Mwenyezi Mungu anakubainisheni Aya. Na Mwenyezi Mungu ni Mjuzi Mwenye hikima. 18

Maelezo ya chini

18 Na Mwenyezi Mungu anakuteremshieni Aya zenye kuonyesha hukumu kwa uwazi dhaahiri. Na Mwenyezi Mungu ni Mkunjufu wa Ujuzi, hapana asicho kijua katika vitendo vyenu. Naye ni Mwenye hikima kwa kila anacho kitungia sharia na kukiumba. Kwani kila sharia zake na uumbaji wake ni kwa mujibu wa hikima.