وَلَئِنۡ أَصَٰبَكُمۡ فَضۡلٞ مِّنَ ٱللَّهِ لَيَقُولَنَّ كَأَن لَّمۡ تَكُنۢ بَيۡنَكُمۡ وَبَيۡنَهُۥ مَوَدَّةٞ يَٰلَيۡتَنِي كُنتُ مَعَهُمۡ فَأَفُوزَ فَوۡزًا عَظِيمٗا ٧٣
Wala'in asābakum fadlum minallāhi layaqūlanna ka al lam takum baynakum wabaynahū mawaddatun yālaytanī kuntu ma'ahum fa afūza fawzan 'azīmā
Na ikIkufikieni Fadhila kutoka kwa Mwenezi Mungu husema, kama kwamba hapakuwa mapenzi baina yenu naye, laiti ni ngekuwa baina yao nikafanikiwa Mafanikio makubwa 73
Maelezo ya chini
73 Na mnapo pata fadhila ya ushindi kutokana na Mwenyezi Mungu, mkapata ngawira za vita, kikundi hicho hicho, kwa kuona maya na kutamani, husema: Laiti tungeli kuwa nao katika vita hivi, nasi tukapata mafanikio ya ngawira nzuri. Na husema haya na hayo kama kwamba hapakuwepo mapenzi yoyote yaliyo wafunga wao na nyinyi.