Surat An-Nisa, aya 72

4:72

وَإِنَّ مِنكُمۡ لَمَن لَّيُبَطِّئَنَّ فَإِنۡ أَصَٰبَتۡكُم مُّصِيبَةٞ قَالَ قَدۡ أَنۡعَمَ ٱللَّهُ عَلَيَّ إِذۡ لَمۡ أَكُن مَّعَهُمۡ شَهِيدٗا ٧٢

Wa inna minkum lamal layubatti'anna fa in asābatkum musībatun qāla qad an'amallāhu 'alayya idh lam akum ma'ahum shahīdā

Na yupo kati yenu anaye bakia nyuma; na ukikusibuni msiba husema: Mwenyezi Mungu kanifanyia kheri sikuwa nao. 72

Maelezo ya chini

72 Na wahadharisheni wanao kaa nyuma wasende nanyi vitani. Miongoni mwa hao mnao ishi nao wakajizuia wasifuatane nanyi kwenda kupigana, mkipatwa na shida na masaibu katika Jihadi, wao wa kikundi hicho, kwa kufurahia yaliyo kusibuni, husema: Mwenyezi Mungu katufanyia kheri kwa kuwa hatukwenda nao vitani.