وَمَن يُطِعِ ٱللَّهَ وَٱلرَّسُولَ فَأُوْلَٰٓئِكَ مَعَ ٱلَّذِينَ أَنۡعَمَ ٱللَّهُ عَلَيۡهِم مِّنَ ٱلنَّبِيِّـۧنَ وَٱلصِّدِّيقِينَ وَٱلشُّهَدَآءِ وَٱلصَّٰلِحِينَۚ وَحَسُنَ أُوْلَٰٓئِكَ رَفِيقٗا ٦٩
Waman yuti'illāha war-rasūla fa ulā'ika ma'al-ladhīna an'amallāhu 'alayhim minan-nabiyyina was-siddīqīna wash-shuhadā'i was-sālihīna wahasuna ulā'ika rafīqā
Na wenye kumt'ii Mwenyezi Mungu na Mtume, hao wa pamoja na wale alio waneemesha Mwenyezi Mungu miongoni mwa Manabii, na Masiddiqi, na Mashahidi, na Watu wema. Na uzuri ulioje kuwa pamoja na watu hao! 69
Maelezo ya chini
69 Na mwenye kumt'ii Mwenyezi Mungu na Mtume kwa kuzifuata kwa unyenyekevu amri zao na kuridhia hukumu yao, basi huyo yu pamoja na alio waneemesha Mwenyezi Mungu kwa uwongofu na kuwawezesha duniani na Akhera. Na watu hao ni Manabii wake, na wafuasi wao walio wasadiki na kuwakubali na wakafuata nyendo zao, na Mashahidi walio kufa katika Njia ya Mwenyezi Mungu, na watu wema watendao mema kwa siri na dhaahiri. Na hapana la kushinda uzuri kuliko kuwa pamoja na watu hawa - haingii mashakani mwenye kukaa nao, wala hayachoshi mazungumzo yao.