Surat An-Nisa, aya 60

4:60

أَلَمۡ تَرَ إِلَى ٱلَّذِينَ يَزۡعُمُونَ أَنَّهُمۡ ءَامَنُواْ بِمَآ أُنزِلَ إِلَيۡكَ وَمَآ أُنزِلَ مِن قَبۡلِكَ يُرِيدُونَ أَن يَتَحَاكَمُوٓاْ إِلَى ٱلطَّٰغُوتِ وَقَدۡ أُمِرُوٓاْ أَن يَكۡفُرُواْ بِهِۦۖ وَيُرِيدُ ٱلشَّيۡطَٰنُ أَن يُضِلَّهُمۡ ضَلَٰلَۢا بَعِيدٗا ٦٠

Alam tara ilal-ladhīna yaz'umūna annahum āmanū bimā unzila ilayka wamā unzila min qablika yurīdūna an yatahākamū ilat-tāghūti waqad umirū an yakfurū bihī wayurīdush-shaytānu an yudillahum dalālā ba'īdā

Huwaoni wale wanao dai kwamba wameamini yale yaliyo teremshwa kwako na yaliyo teremshwa kabla yako? Wanataka wakahukumiwe kwa njia ya upotofu, na hali wameamrishwa wakatae hayo! Na Shet'ani anataka kuwapotezelea mbali. 60

Maelezo ya chini

60 Ewe Nabii! Huwastaajabii hao wanao dai kuwa wanasadiki Kitabu ulicho teremshiwa wewe na vilivyo teremshwa kabla yako wewe, wanataka wahukumiwe katika ugomvi wao kwenye upotovu na uharibifu na hukumu isiyo kuwa ya Mwenyezi Mungu? Na Mwenyezi Mungu amekwisha waamrisha wayapinge hayo, wala wasitake kuhukumiwa kwa hayo. Na Shetani anataka awaachishe Njia ya Haki na Uwongofu, awapotezelee mbali.