وَلِكُلّٖ جَعَلۡنَا مَوَٰلِيَ مِمَّا تَرَكَ ٱلۡوَٰلِدَانِ وَٱلۡأَقۡرَبُونَۚ وَٱلَّذِينَ عَقَدَتۡ أَيۡمَٰنُكُمۡ فَـَٔاتُوهُمۡ نَصِيبَهُمۡۚ إِنَّ ٱللَّهَ كَانَ عَلَىٰ كُلِّ شَيۡءٖ شَهِيدًا ٣٣
Walikullin ja'alnā mawāliya mimmā tarakal-wālidāni wal-aqrabūna walladhīna 'aqadat aymānukum fa'ātūhum nasībahum innallāha kāna 'alā kulli shay'in shahīdā
Na kila mmoja tumemwekea warithi katika waliyo yaacha wazazi wawili na jamaa. Na mlio fungamana nao ahadi wapeni fungu lao. Hakika Mwenyezi Mungu ni Shahidi wa kila kitu. 33
Maelezo ya chini
33 Na wote, wanaume na wanawake, tumewajaalia kuwa wanastahiki urithi wao wa kuwarithi wazazi wawili, na jamaa, na wale ambao mfiliwa amefungamana nao kwa agano ambalo matokeo yake ni kuwa amrithi ijapokuwa si jamaa, na amsaidie pindi anahitajia msaada kuwa ni badala yake. Basi mpeni haki yake kila mwenye haki, wala msipunguze kitu. Hakika Mwenyezi Mungu anakuangalieni kwa kila kitu, na yuko pamoja nanyi, anashuhudia yote myafanyayo.