يُرِيدُ ٱللَّهُ أَن يُخَفِّفَ عَنكُمۡۚ وَخُلِقَ ٱلۡإِنسَٰنُ ضَعِيفٗا ٢٨
Yurīdullāhu an yukhaffifa 'ankum wakhuliqal-insānu da'īfā
Mwenyezi Mungu anataka kukupunguzieni taabu, na mwanaadamu ameumbwa dhaifu. 28
Maelezo ya chini
28 Mwenyezi Mungu anataka kukufanyieni wepesi katika kutunga sharia ambazo ndani yake zina sahala na takhfifu kwenu. Kwani hakika Mwenyezi Mungu amemuumba mwanaadamu kiumbe dhaifu katika kupambana na matamanio na maelekeo ya nafsi. Kwa hivyo yanayo mlazimu katika sharia yana wepesi na wasaa. Na hayo kwa fadhila yake na taisiri yake Mwenyezi Mungu ndiyo anayo walazimisha waja wake.