وَٱللَّهُ يُرِيدُ أَن يَتُوبَ عَلَيۡكُمۡ وَيُرِيدُ ٱلَّذِينَ يَتَّبِعُونَ ٱلشَّهَوَٰتِ أَن تَمِيلُواْ مَيۡلًا عَظِيمٗا ٢٧
Wallāhu yurīdu an yatūba 'alaykum wayurīdul-ladhīna yattabi'ūnash-shahawāti an tamīlū maylan 'azīmā
Na Mwenyezi Mungu anataka kukurejezeni kwenye ut'iifu wake, na wanao taka kufuata matamanio wanataka mkengeuke makengeuko makubwa. 27
Maelezo ya chini
27 Na Mwenyezi Mungu anataka mrejee katika ut'iifu wake, na wale wanao fuata ladha zao, na matamanio yao machafu, miongoni mwa makafiri na waasi, wanataka muwe mbali kabisa na njia ya haki.