Surat An-Nisa, aya 146

4:146

إِلَّا ٱلَّذِينَ تَابُواْ وَأَصۡلَحُواْ وَٱعۡتَصَمُواْ بِٱللَّهِ وَأَخۡلَصُواْ دِينَهُمۡ لِلَّهِ فَأُوْلَٰٓئِكَ مَعَ ٱلۡمُؤۡمِنِينَۖ وَسَوۡفَ يُؤۡتِ ٱللَّهُ ٱلۡمُؤۡمِنِينَ أَجۡرًا عَظِيمٗا ١٤٦

Illal-ladhīna tābū wa aslahū wa'tasamū billāhi wa akhlasū dīnahum lillāhi fa ulā'ika ma'al-mu'minīna wasawfa yu'tillāhul-mu'minīna ajran 'azīmā

Isipo kuwa wale walio tubu, na wakatengeneza na wakashikamana na Mwenyezi Mungu, na wakamtakasia Dini yao Mwenyezi Mungu. Basi hao ni pamoja na Waumini. Na Mwenyezi Mungu atakuja wapa Waumini ujira mkubwa. 146

Maelezo ya chini

146 Isipo kuwa wale katika wao walio tubia, na wakarejea kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu, na wakaungana naye Yeye peke yake, na wakajitakasa, na wakaelekeza nyuso zao kwake, na wakatenda mema. Wakifanya haya basi ndio wanakuwa miongoni mwa Waumini. Watapata malipo ya Waumini. Na Mwenyezi Mungu Mtukufu amekwisha waahidi Waumini malipo makubwa duniani na Akhera.