Surat An-Nisa, aya 117

4:117

إِن يَدۡعُونَ مِن دُونِهِۦٓ إِلَّآ إِنَٰثٗا وَإِن يَدۡعُونَ إِلَّا شَيۡطَٰنٗا مَّرِيدٗا ١١٧

In yad'ūna min dūnihī illā ināthan wa in yad'ūna illā shaytānam marīdā

Wao hawawaombi badala yake Yeye ila wanawake, wala hawamuombi ila Shet'ani aliye asi. 117

Maelezo ya chini

117 Katika upotovu ulio wazi kabisa ambao uko mbali na Haki ni ule wa mwenye kumshirikisha Mwenyezi Mungu. Huyo anaabudu kitu ambacho hakisikii wala hakioni, hakidhuru wala hakinafiishi. Na huita hiyo miungu yake kwa majina ya kike, kama Laata na Uzza na Manaata na mengineyo ya majina ya kike. Yeye hakika kwa hivyo anamuabudu Shetani.