Surat An-Nisa, aya 116

4:116

إِنَّ ٱللَّهَ لَا يَغۡفِرُ أَن يُشۡرَكَ بِهِۦ وَيَغۡفِرُ مَا دُونَ ذَٰلِكَ لِمَن يَشَآءُۚ وَمَن يُشۡرِكۡ بِٱللَّهِ فَقَدۡ ضَلَّ ضَلَٰلَۢا بَعِيدًا ١١٦

Innallāha lā yaghfiru an yushraka bihī wayaghfiru mā dūna dhālika liman yashā'u waman yushrik billāhi faqad dalla dalālā ba'īdā

Hakika Mwenyezi Mungu hasamehi kushirikishwa na kitu. Lakini Yeye husamehe yasiyo kuwa hayo kwa amtakaye. Na anaye mshirikisha Mwenyezi Mungu basi huyo amepotea upotovu wa mbali. 116

Maelezo ya chini

116 Hakika mwisho huu wa kuumiza ni wao hao vile vile, kwani hao ni maadui wa Uislamu. Mfano wake ni mfano wa mwenye kumshirikisha Mwenyezi Mungu. Hakika kila dhambi yaweza kughufiriwa, ila kumshirikisha Mwenyezi Mungu, na kumuabudu mwenginewe asiye kuwa Yeye, na kumpinga Mtume katika Haki. Ni shani ya Mwenyezi Mungu kusamehe madhambi, ila dhambi ya kumshirikisha Yeye katika ibada. Kwa jenginelo lisilo kuwa hili Yeye humsamehe amtakaye. Anaye mshirikisha Mwenyezi Mungu katika ibada na kumtegemea, basi huyo ameipotea Haki, na amekuwa mbali nayo mno; kwani mtu huyo ameifisidi akili yake na nafsi yake pia.