Surat An-Nisa, aya 118

4:118

لَّعَنَهُ ٱللَّهُۘ وَقَالَ لَأَتَّخِذَنَّ مِنۡ عِبَادِكَ نَصِيبٗا مَّفۡرُوضٗا ١١٨

Lla'anahullāhu waqāla la attakhidhanna min 'ibādika nasībam mafrūdā

Mwenyezi Mungu amemlaani. Naye Shet'ani alisema: Kwa yakini nitawachukua sehemu maalumu katika waja wako. 118

Maelezo ya chini

118 Na Mwenyezi Mungu Mtukufu amekwisha mfukuza huyu Shetani kutokana na kivuli cha rehema yake, na amemjaalia awe katika njia ya upotovu. Na Shetani ameapa, na amejichukulia ahadi mwenyewe, kuwa atachota miongoni mwa waja wa Mwenyezi Mungu Mtukufu idadi maalumu awapumbaze kwa upotovu wake na awatie wasiwasi kwa shari yake.