Surat An-Nisa, aya 115

4:115

وَمَن يُشَاقِقِ ٱلرَّسُولَ مِنۢ بَعۡدِ مَا تَبَيَّنَ لَهُ ٱلۡهُدَىٰ وَيَتَّبِعۡ غَيۡرَ سَبِيلِ ٱلۡمُؤۡمِنِينَ نُوَلِّهِۦ مَا تَوَلَّىٰ وَنُصۡلِهِۦ جَهَنَّمَۖ وَسَآءَتۡ مَصِيرًا ١١٥

Waman yushāqiqir-rasūla mim ba'di mā tabayyana lahul-hudā wayattabi' ghayra sabīlil-mu'minīna nuwallihī mā tawallā wanuslihī jahannama wasā'at masīrā

Na anaye mpinga Mtume baada ya kumdhihirikia uwongofu, na akafuata njia isiyo kuwa ya Waumini, tutamuelekeza aliko elekea, na tutamuingiza katika Jahannamu. Na hayo ni marejeo maovu. 115

Maelezo ya chini

115 Na anaye mpinga Mtume s.a.w. baada ya kwisha itambua Njia ya Haki na Uwongofu, na akaifuata njia isiyo kuwa ya Waumini, na akaingia kwenye urafiki na maadui wa Waumini, basi huyo atakuwa na hao. Kwani amekhiari kuwa hao ndio wawe marafiki zake na walinzi wake. Mwenyezi Mungu atakuja mtia Motoni Siku ya Kiyama.