وَيَوۡمَ نَبۡعَثُ مِن كُلِّ أُمَّةٖ شَهِيدٗا ثُمَّ لَا يُؤۡذَنُ لِلَّذِينَ كَفَرُواْ وَلَا هُمۡ يُسۡتَعۡتَبُونَ ٨٤
Wayawma nab'athu min kulli ummatin shahīdan thumma lā yu'dhanu lilladhīna kafarū walā hum yusta'tabūn
Na siku tutakapo wainua kutokana na kila umma shahidi, kisha hawataruhusiwa walio kufuru wala hawataachiliwa kutaka radhi. 84
Maelezo ya chini
84 Ewe Nabii! Mhadharishe kila anaye mkataa Mola wake Mlezi kwa yatakayo tokea Siku tutakapo muinua kutokana na kila umma shahidi wa kuwashuhudia kwa walivyo mpokea Mtume wa Mola wao Mlezi. Na pindi akitaka kafiri kutoa udhuru, hatapewa ruhusa ya kutaka kutoa udhuru. Wala hatapatikana mwombezi wa kumtengenezea maombezi, kwa kutakiwa warejee waache sababu za Mwenyezi Mungu kuwakasirikia. Kwani Akhera sio pahala pa kutubia.