Surat An-Nahl, aya 32

16:32

ٱلَّذِينَ تَتَوَفَّىٰهُمُ ٱلۡمَلَٰٓئِكَةُ طَيِّبِينَ يَقُولُونَ سَلَٰمٌ عَلَيۡكُمُ ٱدۡخُلُواْ ٱلۡجَنَّةَ بِمَا كُنتُمۡ تَعۡمَلُونَ ٣٢

Alladhīna tatawaffāhumul-malā'ikatu tayyibīna yaqūlūna salāmun 'alaykumudkhulul-jannata bimā kuntum ta'malūn

Wale ambao Malaika huwafisha katika hali njema, wanawaambia:Amani iwe juu yenu! Ingieni Peponi kwa sababu ya yale mliyo kuwa mkiyatenda. 32

Maelezo ya chini

32 Na ndio hao Malaika huzichukua roho zao na hali wamesafika na uchafu wa ushirikina na maasi. Na Malaika watawaambia kwa kuwatuza: Amani kwenu itokayo kwa Mwenyezi Mungu! Baada ya hii leo hamtopata la karaha. Na ifurahieni Pepo mtakayo ingia kwa sababu ya vitendo vyema mlivyo vitanguliza katika dunia yenu.