Surat An-Nahl, aya 21

16:21

أَمۡوَٰتٌ غَيۡرُ أَحۡيَآءٖۖ وَمَا يَشۡعُرُونَ أَيَّانَ يُبۡعَثُونَ ٢١

Amwātun ghayru ahyā'in wamā yash'urūna ayyāna yub'athūn

Ni wafu si wahai, na wala hawajui watafufuliwa lini. 21

Maelezo ya chini

21 Na hayo ni vitu visivyo na roho kama maiti, hayana hisiya yoyote, wala hayataharaki, wala hayajui Kiyama kitakuja lini, wala lini watafufuliwa hao wanao yaabudu. Wala si laiki yenu, enyi wenye akili, baada ya haya mkadhani kuwa yatakufaeni kitu hata mkayashirikisha na Mwenyezi Mungu katika kuyaabudu.